Pages

Monday, July 21, 2014

Miss Kanda Mashariki kufanyika Agosti 8 Morogoro


Na Mwandishi Wetu
Mashindano ya kumsaka mrembo kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014) yatafanyika siku ya sikukuu ya Nanenane kwanue ukumbi wa  Nashera Hotel, mkoani Morogoro.

Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo  14 kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa Morogoro chini ya udhamini wa Redds Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.

Tuesday, June 3, 2014

AY & Mwana FA walichokifanya Morogoro


Jumamosi Hii Ay na Mwana FA walikuwa Maeneo ya Morogogo pale Samakisamaki kwa moshow moja matata, Hizi ni picha katika Show hiyo.























Wednesday, May 28, 2014

WAKAZI WA MOROGORO TUMUENZI MANGWEA LEO PALE SAMAKI SAMAKI


Leo ni siku ya marehemu Albert Mangwea. Na kama uko Moro basi si vibaya ukajisogeza pale Samaki Samaki kuanzia saa 10 jioni kwaajili ya kumbukumbu yake. Kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali. Kiingilio ni 5,000/- R.I.P Mangwea 

Sunday, May 4, 2014

TAZAMA PICHA ZA SHOW YA TEMBA NA CHEGE NDANI YA MOROGORO

20140504-135811.jpg
Wasanii wa kizazi kipya kutoka “TMK” Temeke jijini Dar es Salaam, jana siku ya Jumamosi walikinukisha ndani ya Samaki Samaki mji kasoro bahari mitaa ya Kidonda mjini Morogoro. Wakati watanzania wameelekeza Masikio na Macho kwenye KTMA2014, wasanii hawa chini ya MXCarter Entertainment wakishirikiana na NYUMBaNI Park Walifanya show kali kwa ajili ya wakazi wa mjini morogoro ambapo walisheheni eneo la tukio kushuhudia majabali hayo mawili yakiungurumisha ngoma zao mpya na za zamani.
PICHA.
20140504-135756.jpg
20140504-135801.jpg


Tuesday, April 29, 2014

FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI‏

 Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi

Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani

Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.

Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.

 

         


Wednesday, October 30, 2013

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 NDANI YA UWANJA WA JAMHURI MKOANI MOROGORO ILIKUWA NOMA SANAAAAAA



 
 Mmoja wa Wasanii mahiri ambaye anafanya vyema kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,Rachael kutoka THT akionesha umahiri wake wa kuimba na kukata mauno jukwaani,huku shangwe zikiwa zimetawala kila kona ya uwanja usiku huu ndani ya uwanja wa Jamhuri,mkoani Morogoro.
 Sehemu ya mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta 2013 wakishangilia vilivyo usiku huu. 
 Wadau katika pozi la picha usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea ndani ya uwanja wa Jamhuri,mkoani Morogoro.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole akiwa madansa wake wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu. 
 Serengeti fiesta 2013 ni noma saaana usiku huu,kausheni tuu.!
 MKali wa mangoma kutoka Clouds FM,Dj Zero akikamua jukwaani usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea.
 Ni noma saana kwa mashabiki usiku huu wakato tamasha la serengeti fiesta 2013 likiendelea.
 Mwanadada miwngine ambaye anafanya vyema kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Linah akiimba jukwaani usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Jamhuri,mkoani Morogoro.
 Ni burudani asilimia mia kila kona ya uwanja wa jamhuri usiku huu.
 Ni zao lingine la vipaji kuĂ„itia shindano la Serengeti Fiesta supa nyota 2012,ambaye kwa sasa anafanya vyema sana katika muziki wa bongofleva,anaitwa Neylee akiimba jukwaani usiku huu.
 Wadau wakifuatilia yanayojiri kwenye jukwaa la serengeti fiesta usiku huu.
 Na sisi tupo pia na wakazi wa Morogoro noma saana usiku huu.
Pichani kati ni msanii Rachael na skwadi lake wakilishambulia jukwaa la fiesta usiku huu.