Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana,leo walipitia nyumbani kwa Mfalme wa Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro.Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji Afande Sele
Featured Posts
Sunday, August 17, 2014
Friday, August 8, 2014
Monday, July 21, 2014
Miss Kanda Mashariki kufanyika Agosti 8 Morogoro
Na Mwandishi Wetu
Mashindano ya kumsaka mrembo kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014) yatafanyika siku ya sikukuu ya Nanenane kwanue ukumbi wa Nashera Hotel, mkoani Morogoro.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa Morogoro chini ya udhamini wa Redds Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.
Tuesday, June 3, 2014
Wednesday, May 28, 2014
WAKAZI WA MOROGORO TUMUENZI MANGWEA LEO PALE SAMAKI SAMAKI
Leo ni siku ya marehemu Albert Mangwea. Na kama uko Moro basi si vibaya ukajisogeza pale Samaki Samaki kuanzia saa 10 jioni kwaajili ya kumbukumbu yake. Kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbali mbali. Kiingilio ni 5,000/- R.I.P Mangwea
Sunday, May 4, 2014
TAZAMA PICHA ZA SHOW YA TEMBA NA CHEGE NDANI YA MOROGORO
PICHA.
Tuesday, April 29, 2014
FURSA: MAFUNZO YA KUPIGA ALA ZA MUZIKI KUANZA TENA MWEZI MEI
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mazoezi
Action Music Tanzania (AMTz) inatangaza fursa kwa watu wote kujiunga na mafunzo ya kupiga ala za muziki yanayoanza tarehe 3/5/2014, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wanamuziki wa kupiga ala na kufanya maonesho kwa weledi na utaalamu zaidi.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani
Mafunzo yanayotolewa ni pamoja na upigaji wa ala za muziki zikiwemo gita, kinanda, tarumbeta, saxophone, konga, drum set, na upigaji wa ngoma za asili. Pia yatatolewa mafunzo ya ‘body percussion’ yaani matumizi ya mwili katika kutengeneza midundo ya muziki.
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ofisi za AMTZ zilizopo maeneo ya Mwenge mtaa wa Umoja, nyuma ya magorofa ya jeshi na kwenye Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ili kujiunga na mafunzo haya wasiliana nao kwa simu namba 0686928828/0653075791 ili kupata fomu za kujiunga na mafunzo.
Subscribe to:
Posts (Atom)